Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakanusha tozo wanaojifunga nje ya vituo vya huduma za afya

D406c930b840dcfa4531ee8c7d27ee35 Serikali yakanusha tozo wanaojifunga nje ya vituo vya huduma za afya

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dk Stephen Dugange ameeleza kuwa Serikali haijatoa mwongozo wowote kwa watendaji wa huduma za afya nchini kote juu ya kuwatoza pesa wanawake wanaojifungua nje ya vituo vya afya.

Dk Dugange amesema hayo leo akiwa bungeni jijini Dodoma wakati ajikibu swali la Mbunge Grace Tendega lililohoji lini serikali itajenga majengo ya kusubiria huduma za afya kwa wajawazito katika jimbo la kalenga.

Akijibu swali hilo Dk Dugange alisema ni wajibu wa watumishi katika vituo vya huduma kutoa elimu na kuhamasisha wajawazito kuona umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya huduma badala ya kuwalipisha faini wakijifungulia nje ya ivtuo vya huduma.

Chanzo: habarileo.co.tz