Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yajibu matibabu bure kwa wazee mchini

ZAHANATI1 Serikali yajibu matibabu bure kwa wazee mchini

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema matibabu ya wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 bado ni bure kama sera ya serikali inavyoeleza.

Submitted by Elbogast on Alhamisi , 15th Apr , 2021 Moja ya Zahanati nchini

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 15, 2021 bungeni na Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo John Dugange, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Ghati Zephania Chomete, aliyeuliza Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sera ya matibabu bure kwa Wazee wenye umri kuanzia miaka 60 katika Halmashauri za Mkoa wa Mara inatekelezeka.

Serikali inatekeleza Sera ya Afya ya Mwaka 2007 na Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, kwa kufanya utambuzi wa Wazee na kuwapatia huduma mbalimbali za Afya. 

Amefafanua kuwa hadi Disemba 2020 jumla ya Wazee 2,344,747 wametambuliwa sawa na asimilia ya 87 ya makadrio ya Wazee wote nchini. Kati yao Wanaume 1,092,310 na Wanawake 1,252,437. Wazee Wasiojiweza 1,087,008 wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure na wazee 856,052 wamepatiwa kadi za matibabu za Afya ya Jamii (CHF).

Aidha ameeleza kuwa, hadi Februari,2021 Halmashauri za Mkoa wa Mara zimefanya utambuzi wa wazee 70,170 kati ya lengo la kuwatambua wazee 196,000. Kati ya Wazee waliotambuliwa wanaume ni 32,900 na wanawake ni 37,270. Wazee 39,664 wamepewa vitambulisho vya matibabu kati ya wazee 70,170 waliotambuliwa.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri ameeleza kuwa, mkoa wa Mara na mikoa mingine, inaendelea kufanya utambuzi kwa wazee na kuhakikisha wazee wote waliotambuliwa wanapewa vitambulisho vya matibabu bure.

Amemaliza kwa kusema, ''niwaombe Waheshimiwa Wabunge tuendelee tuendelee kuelimisha Wananchi 1,169,000,858.86 kuwa sio wazee wote wanapaswa kupata matibabu bure isipokuwa kwa Wazee wasiokuwa na uwezo.''  

Chanzo: eatv.tv