Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafafanua chanjo ya Covid-19

95d2b43b7ef8dfd60e80ac080e752186.jpeg Serikali yafafanua chanjo ya Covid-19

Sun, 6 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema itakuja na tamko juu mapendekezo ya chanjo ya covid 19 huku ikifafanua kwamba iliyoruhusiwa kuingia nchini ni kwa ajili ya balozi mbalimbali nchini, raia wa kigeni pamoja na wafanyakazi wao.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema serikali imetoa ruhusa kwa balozi na mashirika hayo kutoa fursa ya kuchanja raia wa kigeni pamoja na wafanyakazi ambao baadhi, wameshindwa kurudi kwao kutokana masharti yaliyowekwa.

Alisema hatua hiyo itasaidia raia hao kuwa na sifa za kurudi katika mataifa yao.

“Wafanyakazi katika balozi ni raia wa kigeni ambao wanashindwa kurudi katika mataifa yao kutokana kutochanjwa chanjo ya corona kwa hiyo kama tutaendelea kuwanyima kupata huduma hii itakuwa ni uvunjaji wa haki za binadamu,”alisema Akizungumzia mapendekezo ya kamati ya wataalamu wa afya kuhusu chanjo ya covid 19, alisema

Rais ameelekeza yaandikiwe andiko na yawasilishwe katika Baraza la Mawaziri kujadiliwa na kufanyiwa uamuzi na baada ya hapo, serikali itakuja na tamko .

“Sasa kwenye eneo hili la ugonjwa wa corona kumekuwa na maneno mengi na kujazana hofu bila sababu.

Rais alichoamua ni kuimarisha juhudi za kupambana na janga hili kwa kutoa nafasi kwanza kwa wataalamu wetu wakiongozwa na Profesa Said Aboud kufanya tathimini ya kitaalamu na kuishauri Serikali juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huu,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz