Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaeleza mikakati itakayosaidia mtoto wa kike kutopata mimba shuleni

7648 WILLIAN OLE NASHA TZW

Wed, 9 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Serikali imesema kuwa imepata ufunguzi wa kutambua kwanini watoto wa kike kupata mimba wakiwa shule hivyo imetafuta njia mbadala wa kuwakinga ikiwa ni pamoja na kujenga mabweni.



Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Nasha wakati akijibu swali la Mbunge Suzan Lyimo, serikali inatambua tatizo hilo na kuweka sababu hizo wazi.

“Serikali inatambua tatizo la wanafunzi wa shule kupata mimba wakiwa masomoni kwasababu mbalimbali zikiwemo zile wasizoweza kuhimili, sababu hizo ni kama kubakwa, kutembea umbali mrefu kufuata shule na hivyo kupata vishawishi, Mila na desturi potofu zinazo mlazimisha mwanafunzi kuingia katika ndoa au mahusiano ya kimapenzi na kukosa sababu za msingi kukosa mahitaji ya msingi kutoka kwa wazazi hali mabayo umuingiza mwanafunzi kupata vishawishi ili kupata mahitaji yake,” Ole Nasha.

“Serikali inatambua tatizo la watoto kupata mimba wakiwa shule ikiwa ni pamoja na zile serikali imetekeleza yafuatayo, imefanya marekebisho katika masuala ya Elimu sura 353 toleo la 2002 kupitia sheria marekebisho ya sheria mbalimbali namba 2 ya mwaka 2016 ambayo imeongeza kifungu cha 60 kipengele kikubwa cha ‘a’ ambacho kinatamka wazi kuwa mtu yoyote atakaye mpa ujauzito mtoto wa shule atafungwa miaka 30,” ameongeza.

“Serikali Imezifanya shule zote za kitado cha tano na sita kuwa na mabweni na hosteli kwa wanafunzi wa kike, imehimiza ujenzi wa shule za sekondari kila Kata kwenye maeneo ya wanafunzi wengi ili kuepusha watoto wa kike kutembea umbali mrefu.”

Loading...
Chanzo: bongo5.com