Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaeleza mabilioni yanayookolea kila mwaka

Mollel1 Serikali yaeleza mabilioni yanayookolea kila mwaka

Wed, 24 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inaokoa zaidi ya shilingi bilioni 38 kila mwaka zilizokuwa zikitumika kupeleka wagonjwa nje kutibiwa na sasa wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini baada ya serikali kufanya maboresho katika sekta ya afya.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea taasisi ya mifupa ya Moi, Jengo la wagonjwa wa moyo JKCI na kujionea matibabu mbali mbali yanayofanyika katika hospitali hiyo.

Kwa upande wao madaktari bingwa wa moyo pamoja na viongozi wa taasisi hizo wameeleza changamoto za magonjwa ya moyo na matibabu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live