Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaanika mikakati kupambana na magonjwa yasiyoambukiza

24573 Pic+kiharusi TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imesema inatekeleza mpango mkakati wa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhakikisha dawa za kutibu magonjwa hayo zinafika mpaka ngazi za zahanati.

Imesema tafiti zinaonyesha magonjwa yasiyoambukiza yanashambulia mijini watu 108 kati ya 100,000 ikilinganishwa na vijijini ambako watu 95 kati ya 100,000 kwa mujibu wa tafiti za mwaka 2010.

Hayo yamezungumzwa leo Jumatatu Oktoba 29, 2018 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Kambi wakati akitoa tamko la wiki ya ugonjwa wa kiharusi.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inafanya juhudi mbalimbali kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema na kujikinga na magonjwa hayo ikiwemo kiharusi.

“Pamoja na kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kiharusi, tunazingatia kuwajengea uwezo watoa huduma kwa ngazi zote mafunzo ya mara kwa mara.”

“Kuongeza bajeti ya dawa, vifaa na vifaa tiba ikiwa ni pamoja na kuhakikisha dawa za kutibu magonjwa yasiyoambukiza zinapatikana mpaka kwenye ngazi za zahanati,” amesema Profesa Kambi.

Amesema pamoja na hayo wanashirikiana na wadau katika kuhamasisha wananchi kufanya vipimo vya mara kwa mara na kudhibiti viashiria ambavyo ni magonjwa kama kupanda kwa shinikizo la damu na kuendesha kambi za kupima, kutoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali zikiwemo za vipeperushi na video.

Juni 28, 2018, Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na wadau wengine, waliendesha mjadala wa kwanza kupitia mpango wa Jukwaa la Fikra, lililoangazia magonjwa yasiyoambukiza chini ya kauli mbiu ya “Afya Yetu, Mtaji Wetu”.

MCL ni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti

Chanzo: mwananchi.co.tz