Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaahidi kituo cha afya Chato

Untitled 2 (1) Serikali yaahidi kituo cha afya Chato

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: EATV

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kujenga kituo cha afya kwenye kata ya Minkoto Wilayani Chato ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya  wananchi wa kata tatu zinaozunguka Shamba la Miti Silayo.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Marry Masanja mara baada ya kuzindua mradi wa maji Butengo uliofadhiliwa na wakala wa huduma za misitu TFS uliopo pembezoni mwa shamba la Miti Silayo.

"Mheshimiwa mbunge pia aliomba kituo cha afya swala hili alishalileta mpaka Wizarani, mimi ni shahidi, chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa chini ya Samia Suluhu Hassan na kwa kuheshimu jimbo la Chato na anavyolipenda, kituo cha afya kinaedna kujengwa katika kata ya Minkoto, tutaenda kujenga kituo hiko kwa fedha za TFS", alisema Masanja.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi mhifadhi mkuu wa shamba la Miti Silayo Juma Mwita anasema jumla ya kaya 180 zimeanza kunufaika kupitia mradi huo wa maji uliogharimu zaidi shilingi milioni 22 huku mbunge wa jimbo la Chato Dokta medard Kalemani akiishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma ya maji safi na salama wananchi.

"Wastani wa watu 1080 wananufaika moja kwa moja na mradi huu wa maji, mradi huu mpaka kukamilika kwake umegharimu takribani shilingi za kitanzania milioni 22,161,600",alisema Mwita

"Miradi ya maji ni mingi lakini pamoja na hayo bado changamoto ya maji ipo sasa uwepo wa mradi huu mheshimiw naibu waziri waannchi wa Butengo hawatakusahau wewe na team sako asante na tunashukuru sana",alisema Kalemani.

Baadhi ya wananchi wanaelezea adha waliyokuwa wanaipata  kuchota maji  kwenye visima hasa kipindi cha kiangazi.

"Mwanzo tulikuwa tunapata maji sehemu za mbugani mbugani na mito midogo midogo sio mikubwa sana kivile kwa vile yamekuja haya maji kidogo unafuu upo sio kama kipindi cha nyuma tulivyokuwa",alisema kavuna

"Wakati mwingine sisi wanawake tulikuwa tunaamka usiku kufata maji sehemu mbali mbali labda unakuta huko maji, unakuta foleni",alisema Joseph.  

Chanzo: EATV