Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania haina taarifa ukosefu wa vifaa hospitali ya Morogoro

57372 Vifaapic

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali haina taarifa za upungufu wa vifaa na mashine za vipimo lakini wameahidi kufuatilia.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Mei 14, 2019 na naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustin Ndugulile bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Devotha Minja.

Katika swali lake, Minja alitaka kujua ni lini Serikali itaisaidia hospitali ya mkoa wa Morogoro ambayo haina Oxygen, karatasi za kuchukulia picha za X-ray mashine na vifaa vingine muhimu kwa miezi minne sasa.

Dk Ndugulile amesema jambo atalifuatilia kuanzia leo kwani alikuwa amelisikia leo bungeni lakini ni muhimu.

Katika swali la msingi mbunge wa viti maalum (CCM),  Ester Mahawe amehoji ni lini Serikali itapandisha hadhi kituo cha afya cha Dongobeshi ili kiweze kuwahudumia wananchi wa Mbulu pamoja na kuongeza watumishi wa Afya katika kituo hicho.

Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Josephat Kandege amesema kituo hicho kinahudumia wakazi 30,000 wa tarafa ya Dongobeshi na maeneo ya jirani.

Pia Soma

Amesema mwezi Machi 2018, serikali ilitoa sh 400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ambayo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni ikiwemo wodi ya akina mama,upasuaji, maabara,nyumba ya utumishi na sehemu ya kuhifadhia maiti.

Chanzo: mwananchi.co.tz