Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali, wadau wazindua huduma nafuu kwa wagonjwa wa kisukari

Wagonjwapicc  Data Dkt Makubi akiainisha mpango wa iCARE

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari (TDA) na shirika la Novo Nordisk wamezindua mpango upatikanaji wa huduma nafuu za insulin kwa wagonjwa wa kisukari wa aina ya kwanza wengi wao wakiwa watoto.

Mpango huo unaofahamika kama ‘iCARE’ tayari umeshafika katika nchi kadhaa za Afrika unalenga kuwafikia zaidi ya wagonjwa 5,900 nchini Tanzania kwa kuwawezesha kupata dawa aina ya insulin kwa unafuu katika mikoa tisa, ukifanya kazi katika vituo 75 katika ngazi za wilaya, mikoa na taifa.

Mpango huo pia unatarajiwa kuwajenga uwezo watoa huduma wa afya 350 katika ngazi mbalimbali hasa zahanati na vituo vya afya ili vituo hivyo viweze kutoa huduma na matibabu ya kisukari katika maeneo yao.

Akizungumzia mpango huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makumbi amesema umekuja wakati muafaka na utaisaidia serikali kupunguza mzigo wa gharama za tiba hiyo ambayo ni muhimu zaidi kwa watu wenye kisukari.

“Mpango huu unaleta unafuu kwetu kwani unawazesha wagonjwa wa kisukari wenye kuhitaji dawa ya insulin kumudu gharama, bahati mbaya kisukari cha aina ya kwanza wengi wanaogundulika ni watoto na wanahitaji kuchoma dawa hizi kila siku katika maisha yao yote hivyo ni muhimu zikipatikana kwa unafuu,” amesema Profesa Makubi.

Mwenyekiti  wa TDA Profesa Andrew Swai amesema Tanzania ina watoto 4000 ambao wanahudhuria kliniki za kisukari wakihitaji dawa ya insulin kila siku hivyo kupatikana kwa gharama nafuu inaenda kuwapunguzia makali.

Advertisement Amesema hadi sasa bado kuna watu wengi ambao hawajijui kuwa wana ugonjwa wa kisukari na matokeo yake wanakwenda hospitali katika hatua za mwisho hali inayosababisha kushindwa kutibika na kuishia kupoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live