Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuzipatia CT-Scan hospitali zote za rufaa nchini 

7e400c33ff748816366a4d9bd6424112 Serikali kuzipatia CT-Scan hospitali zote za rufaa nchini 

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, amesema ndani ya kipindi cha miezi sita serikali imepanga kununua na kusambaza mashine za kufanyia uchunguzi wa mwili kwa mionzi (CT-Scan) kwenye hospitali zote za rufaa za mikoa nchini.

Alisema hayo juzi wakati akifunga Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.

Alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa serikali kuboresha huduma za afya nchini.

“Kwa sasa ni hospitali mbili pekee nchi nzima zenye mashine za CT-Scan kitu ambacho kinawapa wakati mgumu wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo kwenye maeneo mengi, kuongeza gharama na msongamano katika upatikanaji wa huduma hiyo,” alisema.

Dk Mwigulu alisema mbali na mashine hizo, pia serikali itahakikisha huduma ya X-Ray inaanza kutolewa kwenye hospitali zote za wilaya nchini na huduma ya MRI kutolewa kwenye hospitali zote za kanda.

“Tayari fedha zimeshatengwa na utekelezaji unatarajiwa kufanyika ndani ya miezi sita kuanzia sasa ambapo utaenda sambamba na ugawaji wa magari yenye mitambo ya kuchimba maji kila mkoa ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji nchini,” alisema Dk Mwigulu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, aliishukuru serikali kwa kuendelea kuongeza bajeti ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ambapo mkoa huo umepokea Sh bilioni saba kwa ajili hiyo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2021/2022.

Chanzo: www.habarileo.co.tz