Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuzindua 'Booster' chanjo ya COVID-19

COVID 19 Vaccine Booster Serikali kuzindua 'Booster' chanjo ya COVID-19

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya hivi karibuni itazindua ‘Booster’ dozi ya nyongeza ya Covid-19 ili Wananchi waweze kuongeza kinga zaidi dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 na kusema kuwa ni hiari kwa Mtu yeyote kwenda kupata chanjo hiyo.    Ummy amesema kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2022 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya wamefanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 na kufikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kupata dozi kamili ya chanjo dhidi ugonjwa huo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya hivi karibuni itazindua ‘Booster’ dozi ya nyongeza ya Covid-19 ili Wananchi waweze kuongeza kinga zaidi dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 na kusema kuwa ni hiari kwa Mtu yeyote kwenda kupata chanjo hiyo.    Ummy amesema kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2022 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya wamefanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 na kufikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kupata dozi kamili ya chanjo dhidi ugonjwa huo. Ummy amesema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba 2022 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Jijini Dodoma.   Ameema hadi kufikia Desemba 31, 2022 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokelewa ambapo dozi 41,581,670 zilikuwa zimesambazwa nchi nzima huku kiasi cha chanjo zilizosalia kwenye bohari ya kutunzia chanjo ni 5,266,850 ambazo zote ni aina ya J.J.   Kuhusu huduma za chanjo kwa Watoto, Waziri Ummy amesema huduma hizo zimeendelea kutolewa kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja kwa chanjo ya Penta3 ambayo hutumika kama kipimo kikuu ilifikia asilimia 107 ukilinganisha na mwaka 2021 iliyofikiwa kwa asilimia 96.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live