Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuweka kliniki maalum za wagonjwa wa mifupa Zanzibar

Serikali Kuweka Kliniki Maalum Za Wagonjwa Wa Mifupa Zanzibar Serikali kuweka kliniki maalum za wagonjwa wa mifupa Zanzibar

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara inakusudia kuweka kliniki maalum za wagonjwa wa mifupa (SICKEL CELL) katika hospitali za Wilaya ili kupunguza changamoto ya kufuata huduma hizo katika hospitali ya Mnazimmoja.

Ameyasema hayo wakati akipokua akizungumza na madaktari pamoja na wazazi wa watato wenye ugonjwa huo katika maadhimisho ya siku ya sikoseli yaliofanyika Skuli ya maandalizi Kidutani Mjini Unguja.

Alisema kwa sasa zanzibar ina wagonjwa zaidi ya mia mbili wanaojulikana wa sikoseli hivyo hatua ya kuanzishwa kliniki katika hospitali za Wilaya kutawapunguzia mzigo Hospitali ya Mnazimmoja na kuwaacha wakihudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali za Wilaya na Mkoa.

Akizungumizia suala la upatikanaji wa damu salama ambayo ndio hitajio kubwa la wagonjwa hao Waziri mazrui alisema upatikanaji wa damu bado ni mdogo kulingana na mahitaji hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kushajihishana kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu hasa watoto wanaoishi na ugonjwa wa mifupa kwani wao ndio wahitaji wakubwa. “Ipo haja sasa ya kuchangishana damu kama tunavyochangishana katika mambo mengine ili tuokoe maisha ya wagonjwa wa sikoseli na kujiwekea akiba sisi wenyewe kwani pia niwahitaji watarajiwa.” Alisisitiza Waziri Mazrui.

Mapema Waziri mazurui aliutaka Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuhakikisha maadhimio waliojiwekea yanatimia ikiwemo kujenga na kuimarisha jumuiya za kilimwengu za seli mundu pamoja na kurasimisha uchunguzi wa watoto wachanga wanapozaliwa ili kujua Hali ya ugonjwa wa sikoseli.

Alifahamisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika si kwaajili ya kufurahia uwepo wa ugonjwa huo Bali ni kwa ajili ya kujuana , kuweka na kusimamia mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika kuhakikisha watoto hao wanatambulika na kupata misaada mbalimbali Waziri Mazrui aliwataka Madaktari kwa kushirikiana na wazazi wa watoto hao kuanzisha jumuiya maalum ili kuweza kutambulika na kupata misaada mbalimbali kutoka kwa wafadhili wa nje na ndani ya nchi.

“Kipimo kimoja cha kupima selimundu kwa mtoto mchanga kinagharimu elfu13 , tukiwa na jumuiya kutapelekea kupata Misaada angalau wa hivi vipimo vya kuchunguzia ugonjwa huu kwa watoto wetu mara tu wanaozaliwa kama tunavyowachunguza virusi vya ukimwi” alishauri waziri mazurui. vile vile aliwataka wanandoa watarajiwa kuchunguza afya zao kwa kuangalia hali ya sikoseli kabla ya ndoa kwani endapo wazazi watakua na ugonjwa huo Wana nafasi kubwa ya kurithisha kizazi kitakachozaliwa.

“Tuache kuendekeza mapenzi ifike wakati tuchunguzane sikoseli kama tunavyochunguzana ukimwi kabla ya ndoa,hii itasaidia kupungua kwa watoto wanaorithishwa sikoseli kutoka kwa wazazi wao” alisisitiza Mazurui.

Sambamba na hayo Waziri Mazrui aliwashukuru madaktari kwa kuwapatia huduma bora watoto hao pamoja na wazazi wanaoendelea kuwatunza kwani kuna baadhi ya wazee huwatelekeza mara baada ya kugundua ni wagonjwa.

Nao wazazi wa watoto wanaoishi na ugonjwa huo Wameiomba Wizara kutowakuwachanganya watoto wao katika wodi ya watu wazima wafikapo umri wa miaka 13 kwani bado ni wadogo na wanahitaji kuwa karibu na wazazi.

Aidha, waliushauri Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuweka wodi maalum kwaajili ya watoto wenye ugonjwa huo wenye umri wa kuanzia miaka 13 Hadi 18 ili waweze kuwa nao karibu katika kipindi kigumu cha ugonjwa.

Dunia huadhimisha siku ya Ugonjwa wa SICKEL CELL kila ifikapo Juni 19 kwa lengo la kuwajengea uelewa na kufanya ukaguzi wa afya kwa watu mbali mbali ili kuchukua tahadhari za mapema juu ya ugonjwa huo, Kauli mbiu “VUNJA MDUARA,PIMA JUWA HALI YAKO YA SIKOSELI”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live