Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amethibitisha kuwepo kwa vifo vingi vinavyotokana na Ugonjwa wa Corona, huku akiwataka wananchi kuwa watulivu kwani takwimu hizo zipo karibu kutolewa na Wizara ya Afya.
Ameyasema haya leo akiwa kwenye ziara yake mkoani Mara, ambapo alisisiiza kuwa idadi hiyo itatolewa kwa weledi mkubwa.
"vifo vipo vitatolewa, vifo vipo vya kutosha, ndio tunaandaa na kamati, takwimu sisi tunazo, muwe wavumilivu"
Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, takwimu za waliogua na kufariki zimekuwa haziwekwi wazi mara kwa mara, hatua hii ya kuweka wazi idadi ya vifo vya corona inatajwa kama hatua nzuri ya kupambana na ugonjwa huo.
Hata hivyo aligusia pia suala la vyeti kwa waliochoma chanjo ya Corona, kuwa wameborosha mfumo wa kieretroniki utakao wawezesha watu wote waliochoma chanjo hiyo kupata vyeti hivyo kwa njia ya mtandao.