Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kupunguza gharama za matibabu ya figo

Figoo (600 X 400) Serikali kupunguza gharama za matibabu ya figo

Tue, 21 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ina mpango wa kupunguza gharama zinazotumiwa na wananchi katika kusafisha figo kwa kununua vifaa na vitendanishi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji .

Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge Mariam Nassoro Kisangi aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali kusaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu.

Naibu Waziri Mollel amesema muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote utakapokamilika utakuwa suluhisho la kudumu kwa wananchi nchini wanapotaka kupata huduma ya matibabu.

Aidha Naibu Waziri Mollel amesisitiza sera ya afya ya nchi inaelekeza hamuna mtanzania anayetakiwa kufa kwa sababu ya kukosa fedha hivyo serikali imekuwa ikitoa msamaha kwa wasio na uwezo na waliotimiza vigezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live