Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kupeleka milioni 300 za Vifaa Tiba Njombe

WATUHUMIWA Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu, ameahidi kutoa vifaa tiba vyenye thamani ya Milioni 300 kwa ajili ya kituo cha afya Makowo halmashauri ya mji wa Njombe kilicho kamilika kwa asilimia 100 tayari kwa ajili ya kuweza kutoa huduma ya matibabu.

Ummy ametoa ahadi hiyo alipofika katika halmashauri hiyo na kuzungumza na watumishi pamoja na kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho cha afya kilichopo katika kata ya Makowo.

"Naahidi vifaa tiba vya shilingi milioni 300 kuwaunga mkono wana Makowo na jambo la pili la watumishi kwa bahati nzuri tutapata ajira mpya kwa hiyo tutahakikisha tunaweka orodha kuwa tuna kituo cha afya Makowo kinahitaji watumishi kwa hiyo na watumishi wa afya tunawaletea"alisema Ummy Mwalimu.

Aidha waziri Ummy ameahidi gari ya kubeba wagonjwa katika kituo hicho kutokana na ombi kubwa la wakazi wa kata hiyo wanaosafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

"Tunaahidi gari ya wagonjwa Land Cruser na mama Samia amesema Kazi iendelee kwa hiyo tunawaletea gari ya wagonjwa lakini swala la umeme nimelipokea naenda kuwa barozi wenu kwa waziri wa nishati" aliongeza Ummy.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo alisema alikuwa akisumbuliwa na viongozi wa halmashauri hiyo juu ya Mambo hayo matatu ya muhimu katika kituo cha afya ili kiweze kuanza kutoa huduma kea wananchi.

"Watu wanne akiwemo diwani wa hapa, mkurugenzi pamoja Mbunge wamekuwa wakinisumbua sana kwa ajili ya vifaa tiba,gari la kubeba wagonjwa,umeme na watoa huduma za afya. Nina uhakika wananchi wa Makowo wanakwenda kupona"

Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala licha ya kupongeza juhudi za wananchi katika ujenzi wa kituo hicho cha afya na kuahidiwa kuletewa vifaa tiba ili kiweze kuanza kutoa huduma,ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Kituo cha afya Makowo kilichokamilika mkoani humo kinatajwa kujengwa kwa ghalama ya milioni 598 huku zaidi ya milioni 40 zikiwa zimetokana na nguvu ya wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live