Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga ‘hospitali’ inayotembea ndani ya Ziwa Victoria

RdbKQSYn.jpeg Serikali kujenga ‘hospitali’ inayotembea ndani ya Ziwa Victoria

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hafla ya kutia saini utekelezaji wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh4 bilioni imefanyika jijini Mwanza, leo Desemba 22, 2023.

Mkataba huo ambao utekelezaji wake utakamilika ndani ya miezi 12 umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tasac, Mohamed Salum na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Loca Muhendis Link ya Uturuki, Hidayet Cetin ambao kila mmoja ameahidi utakamilika ndani ya muda uliopangwa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema ujenzi wa boti hiyo ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa vituo sita vya utafutaji na uokozi ndani ya Ziwa Victoria, kwa lengo la kuongeza uwezo na utayari wa utafutaji na uokozi wakati wa majanga ya ajali za majini.

Mradi wa ujenzi wa vituo vya utafutaji na uokozi ndani ya Ziwa Victoria unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh25.8 bilioni.

Kituo kikuu cha utafutaji na uokozi kinajengwa eneo la Ilemema, jirani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza huku vituo vingine vitajengwa maeneo ya Bandari za Bukoba, Musoma na Ukerewe.

Vituo vingine vitajengwa eneo la Magarini Wilaya ya Bukoba, Chato Darajani na Kakukuru wilayani Ukerewe.

Miongoni mwa ajali zilizowahi kutokea kwa upande wa Tanzania ni ya meli ya MV Bukoba iliyotokea Mei 21, 1996 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 800 na ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichotokea pwani ya kisiwa cha Ukara, Septemba 20, 2018 na kukatisha maisha ya watu zaidi ya 225.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live