Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga ICU 72 nchi nzima

Ynews 252813850 Serikali kujenga ICU 72 nchi nzima

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa fedha na mipango Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inakwenda kujenga vyumba vya wagonjwa mahututi(ICU) vipatavyo 72 katika Kila hospitali za rufaa, mikoa na baadhi ya wilaya.

Amesema hayo Leo Oct 10,2021 jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa kampeni ya maendeleo Kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.

"Tunaenda kujenga ICU kwa mpigo katika kila wilaya, mkoa, kutoka zilizokuwepo 5 hadi 72, ili kuweza kuokoa maisha ya watu, tunakwenda kununua vifaa vya kisasa vitakavyotumika katika ICU hizo na tutajenga miundombinu ya kutolea huduma za dharura(EMD)katika hospitali za Taifa, Rufaa, Mikoa na Wilaya jumla zinazenda kuongezeka hospitali 105 kwa mpigo kutoka hospitali 10 zilizokuwa na facility hizo" Waziri wa Fedha

Ameongeza kusema kuwa tayari fedha za kutekeleza miradi hiyo zimeshatengwa na kuwa kilichobki ni utekelezaji ili kueza kunusuru maisha ya watanzania kwa kuboresha huduma za afya nchi nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live