Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuja na mwarobaini matibabu ya figo

Wagonjwa Msigwa Data Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mahitaji ya huduma ya kusafisha damu (Dialysis) yakiongezeka nchini huku gharama zake zikiwa kubwa na kuwa kikwazo, Bohari ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingia mkataba na watengenezaji wa mashine na vitendanishi vya huduma hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Februari 13, 2022 na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Unguja visiwani Zanzibar.

“Baada ya majadiliano na wazalishaji, MSD imeweza kuafikiana nao kwa bei ya Sh57, 000 kwa seti moja ya vitendanishi ambavyo hapo awali MSD ilikuwa inainunua kwa gharama ya Sh185, 000. Sasa kutokana na kupungua kwa gharama za vitendanishi MSD itaweza kuwasambazia watoa huduma kwa gharama ya Sh115, 000 kwa seti moja ya huduma iliyokamilika ikiwa imejumuisha gharama zote,” amesema

Amesema awali gharam zote ikujumuishwa na usafirishaji wa vifaa hivyo hadi katika hospiati husika ilikuwa ikigharimu kati ya Sh200, 000 hadi Sh250, 000.

Hali hiyo italeta ahueni kwa wagonjwa ambapo hospitali zitatoa huduma hizo kwa gharama isiyozidi Sh150, 000 kwa awamu moja, hivyo kuokoa zaidi ya Sh12.9 milioni kwa mgonja mmoja kwa mwaka.

Amesema kwa sasa jumla ya mashine 10 kutoka kwa watengenezaji watatu zimesimikwa katika Hopsitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Advertisement Wizara ya Afya inatekeleza Mpango wa II wa kuziwezesha Hospitali za Rufaa za Mkoa nchini kuanza kutoa huduma hiyo ya dialysis.

Kwa mujibu wa Msigwa, hospitali 15 zimeshafanyiwa uhakiki wa kuanza kutoa huduma hiyo.

“Hivi navyoongea nanyi wataalamu wetu wapo katika mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma hizi kwa maana ya mafunzo ya kutumia vifaa vya dialysis na pia ukarabati wa majengo unaendelea,” amesema

Msemaji huyo wa Seriklai amesema MSD imeshanunua mashine 161 ambazo zitasimikwa kwenye Hospitali hizo za Rufaa za Mikoa, kila hospitali itafungiwa mashine takribani 10, pamoja na mashine moja ya kusafisha maji.

Mbali na hayo, pia MSD imeajiri wataalamu wa vifaa tiba tisa ambao wamekwishapata mafunzo ya kufunga, kufundisha na kufanyia matengenezo mashine hizo, na wataalamu hao ndio watatumika kufunga, kutoa mafunzo sambamba na kuzifanyia matengenezo.

Amesema katika mpango huo hata hapa Zanzibar, MSD inashirikiana na Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS) ya kuleta dawa na vifaa tiba, na hivyo manufaa haya yatapatikna kila upande.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live