Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuipitia upya mitaala ya wakunga

Wakunga Serikali Serikali kuipitia upya mitaala ya wakunga

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetaja sababu mbili za kupitia mitaala ya fani ya wakunga baada ya kubaini kuwa wengi wao wana viwango vya chini ukilinganisha na soko linavyotaka.

Lengo ni kuwa na wakunga wenye sifa zitakazowezesha wafikie viwango vya kimataifa ili waweze kuajilika kwa nchi huku sababu ya pili ikitajwa kuwa ni hofu ya kiwango cha juu cha vifo vitokanavyo na vizazi hai.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi wakati akifungua Kongamano la Kisayansi la wakunga katika siku yao ambalo limefanyika jijini Dodoma.

Profesa amesisitiza kuwa kiwango cha vifo vitokana na uzazi hai siyo ya hali ya juu lakini hata kwa kiwango kilichopo bado kingepaswa kuwa chini ya hapo kwani miundombinu ya sasa ni mizuri ukilinganisha na zamani.

Kingine ametaja idadi ya wakunga kuwa wengi lakini hawana ajira hivyo ni wakati sasa serikali kuanza kutafuta kazi nje ya nchi na kwa walio tayari watapelekwa kufanya kazi huko.

“Kwa hiyo ni lazima tuwe na viwango vinavyokubalika, vinginevyo una mpeleka mtu na nguvu na nia ya kufanya kazi lakini utakuta anashindwa kwenye usaili,” amesema Profesa Makubi.

Advertisement Mkutano huo uliokutanisha idadi kubwa ya wakunga ulidhaminiwa na Taasisi ya Aga Khan, Muhimbili na Hospitali ya Kailuki ukiwakusanyisha wadau kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hata hivyo Serikali imesema haina takwimu sasa za wakati huu kuhusu vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua lakini hadi 2015/15, kulikuwa na vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000.

Profesa Makubi amesema idadi ya wakunga nchini ni wengi licha ya kuwa hawajatosheleza lakini miundombinu yao ni salama ukilinganisha na miaka ya nyuma lakini inashangaza kuona bado idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi viko juu.

Amesema zamani kulikuwa na uhaba wa wakunga lakini vifo vilikuwa chini ukilinganisha na idadi ya wataalamu kwa sasa lakini idadi ya vifo bado inaonekana kuwa juu.

Mkufunzi wa Ukunga katika Chuo cha Aga Khan Loveluck Mwasha alikiri kuwepo kwa mapungufu kwa wakunga wa siku hivi hizi akisema jambo hilo linatakiwa kubebwa na kila mtu vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya.

Mwasha ambaye ni Makamu wa rais wa baraza la wakunga Tanzania, alisema kongamano hilo la kisayansi ndilo litakalokuwa na majibu ya nini kifanyike huku akishauri kuwa mitaalamu iangaliwe na vyuo vibanwe kusajili idadi ya wanafunzi wanaotakiwa siyo zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live