Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufanya utafiti wa tatizo la nguvu za kiume

58401 Pic+rijali+2

Sun, 19 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema Serikali itafanya utafiti wa tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwa sababu kwa muda mrefu wanaume wamekuwa wakitafuta suluhisho kwa kificho, hivyo kukosa taarifa sahihi.

Amesema wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), inafanya utafiti wa afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu ya ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kwa kiasi gani nchini.

Dk Ndugulile alisema kwa kipindi kirefu Serikali imekuwa ikitilia mkazo afya ya uzazi kwa wanawake tu.

“Hatujafanya utafiti wa kina kujua tatizo ni kubwa kiasi gani, ukiangalia takwimu za uzazi Tanzania kwa maana ya ongezeko la watu na idadi ya kinamama kukua, unaona kabisa hatuna shida,” alisema.

Hata hivyo, alisema takwimu za kidunia, sayansi inaonyesha kuwa wanaume wengi wana matatizo ya nguvu za kiume.

Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo kutoka Hospitali ya Taaluma na Tiba, Mloganzila (MAMC), Dk Deogratius Mahenda, anasema zamani wagonjwa wengi waliofika hospitali kupata matibabu walikuwa wanaume wa umri mkubwa (Lakini) miaka ya karibuni kuna ongezeko la vijana walio chini ya miaka 30.

Habari zinazohusiana na hii

Dk Mahenda alisema vijana wengi wanaofika kupata matibabu huwa na historia ya kujichua, msongo wa mawazo, uzito uliopitiliza au lishe duni. Alisema kujichua ni moja ya tatizo kubwa na iwapo kijana akianza mapema uwezekano wa kukosa nguvu za kiume utakuwa mkubwa.

Visababishi vingine

Dk Mahenda alitaja visababishi vikuu vinne kuwa chanzo cha kupungua kwa nguvu za kiume ikiwemo tatizo la kisaikolojia, magonjwa yanayoathiri mwili, mtindo wa maisha na kujichua ambayo imeonekana kuwaathiri zaidi vijana.

Alisema msongo wa mawazo limekuwa ni tatizo kubwa linalowaathiri wanaume wengi kisaikolojia huku akisisitiza kuwa ili nguvu za kiume zipatikane, mwanaume anatakiwa kuwa sawa kiakili ili homoni za kiume zifanye kazi. “Magomvi ya mara kwa mara kwa wanandoa huchangia tatizo lakini pia hali duni kimaisha inamfanya anakuwa na mawazo mengi,” anasema.

Alisema tafiti nyingi zimebaini kuwepo magonjwa yanayosababisha hitilafu kwenye mishipa ya damu na kuwa chanzo cha ukosefu wa nguvu za kiume.

Alitaja shinikizo la damu, mafuta mengi mwilini na kisukari kuwa ni magonjwa yanayoathiri mishipa ya damu na kusababisha mfumo wa ufanyaji kazi mwili kuwa hafifu. “Magonjwa kama uti wa mgongo na pingili za mgongo na wakati mwingine magonjwa ya ajali na selimundu ambao wapo wengine damu ikiganda inakuwa vigumu kwenda tena chini na hivyo kusababisha tatizo hilo kwao.”

Anazitaja dawa kuwa chanzo kingine cha tatizo, umezaji dawa mara kwa mara hasa za magonjwa ya presha na kisukari na matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi huchangia tatizo.

Wataalamu zaidi waeleza

Wataalamu wanafafanua kuwa ili nguvu za kiume zipatikane, mwanaume anatakiwa kutokuwa na hitilafu yoyote katika mfumo wa damu, sambamba na magonjwa yanayoathiri mishipa ya damu.

Mwananchi limefanya mahojiano na wataalamu wa fiziolojia, wataalamu wa mfumo wa mkojo ‘urology’, wataalamu wa lishe na watafiti ambao wamefafanua hatua kwa hatua visababishi vinavyochangia mwanaume kupoteza nguvu za asili za kiume na kuainisha suluhu na tiba.

Daktari bingwa wa fiziolojia ya homoni na mazoezi katika Chuo Kikuu cha Afya Kishiriki cha Sayansi Muhimbili (Muhas), Frederick Mashili anataja saikolojia na kwamba ubongo unahusika katika tendo hilo, lakini kikubwa ni vichocheo yaani homoni za kiume ambazo kiwango chake kinaongezeka zaidi nyakati za asubuhi.

“Kwenye uume kuna mishipa mikubwa ya damu, upo kama sponji hivyo mwanaume anavyojengeka kisaikolojia kuwa tayari kwa lile tendo damu hutoka katika maeneo mengine ya mwili na kushuka chini. Damu ikienda katika uume hushibisha ile mishipa inatanuka, uume hurefuka na kunenepa na ndipo nguvu za kiume hutokea,” anasema.

Dk Mashili anataja sababu kubwa inayoleta matatizo kwa wengi kuwa ni mishipa ya damu, “hapa ndiyo unakutana na dawa za kuongeza nguvu ambazo kazi yake hushusha damu kwenye uume.”

Anasema kabla mtu hajatumia dawa hizo ni lazima apate ushauri wa daktari.

Chanzo: mwananchi.co.tz