Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufanya tathmini gharama za matibabu

Gharama Pic Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Wizara ya Afya imesema inadhamiria kufanya tathmini ya kina ya gharama za matibabu ili kupunguza mzigo kwa Watanzania.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Agosti 10, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika mkoani Njombe.

Waziri Ummy amesema kama ilivyofanyika kwenye kuweka ruzuku katika mbolea, Wizara ya Afya nayo imedhamiria kupunguza mzigo wa gharama za matibabu.

“Sasa hivi kumuona daktari ni Sh15,000 hivi fedha zote hizi ni za nini, timu yangu inafanya tathmini tutashusha gharama za kumuona daktari. Afya ni huduma na sio biashara.

“Sekta ya afya tuna deni kubwa la kupunguza gharama za kupata matibabu, tunao wajibu katika hili na lazima tulifanyie kazi tuwapunguzie mzigo Watanzania wa kulipa fedha nyingi kupata huduma kwenye hospitali zetu,”

Akizungumzia matibabu ya wazee kama ilivyobainishwa na Sera ya Afya, Waziri Ummy amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wazee wasio na uwezo wanapata vitambulisho vya matibabu bure.

“Vitambulisho hivyo viheshimiwe, sio mzee anakuja unamwambia dawa hakuna wakati mzigo wa dawa umeshushwa. Hatutaki visingizio visivyo vya lazima,” amesema Waziri Ummy.

Chanzo: Mwananchi