Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuanza na Mkoa wa Dodoma kufanya tafiti kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi

8501 1 1 2 TZW

Thu, 31 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Serikali imesema inafanya utafiti Maalum kujua kwanini baadhi ya mikoa maambukizi ya Ukimwi yameongezeka ukiwepo mkoa wa Dodoma.



Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Masoud aliehoji, 

Kwa kuwa hali ya Maambukizi katika jiji la Dodoma unaongezeka kwa kasi sana na kwa kuwa katika baadhi ya Nchi duniani wanatumia njia Mbadala ile ya kuweza kutumia mate kuweza kutambua wale waathirika wa VVU, naomba serikali ituambie ina mkakati gani wa ziada kuleta mkakati huu mpya wakuwatambua waliopata athari hii VVU kwakutumia njia ya kutumia mate na hasa tukianzia Mkao huu wa Dodoma?

“Ni kweli Mkoa wa Dodoma Maambukizi yamepanda kutoka asilimia 2.4  hadi asilimia 5 sawa sawa kwa mkoa wa Tanga na Mkoa wa Mwanza, kwahiyo sambamba na hilo tunafanya utafiti Maalum ya kwanini baadhi ya mikoa maambukizi ya Ukimwi yamepanda mwaka 2012, mpaka 2016/17, “amesema Ummy.

Loading...
Chanzo: bongo5.com