Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuajiri watumishi 500 kada ya afya

Ajira Mpyaaaaa Serikali kuajiri watumishi 500 kada ya afya

Sat, 30 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kuajiri watumishi 500 wa kada ya afya katika halmashauri ili kukabiliana na uhaba wa watumishi kwenye Zahanati, Vituo vya afya na hospitali nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana Ijumaa Septemba 29,2023 katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga ambapo alifunga mafunzo kozi namba 01/2023 kwa askari wa Uhamiaji katika Chuo cha Mafunzo ya Uhamiaji cha Raphael Kubaga wilayani Mkinga na kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Hospitali ya wilaya Handeni.

Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kibali kwa Wizara ya Afya kufanya mchakato wa kuajiri watumishi hao na watapelekwa kwenye halmashauri.

Amesema Serikali inafahamu kuhusu changamoto ya watumishi wa idara ya afya kwani imetoa pesa nyingi kwenda katika halmashauri kujenga zahanati.

Naibu Waziri wa Afya, Godwin Molel amesema Wilaya ya Handeni imepokea zaidi ya Sh15 bilioni zilizotolewa na Serikali na wadau kwenye shughuli za maendeleo hasa kwenye idara ya afya.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba kwa upande wake amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwasababu wamesaidia miradi mingi.

Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya Handeni, Kanansia Shao amesema bado wanakabiliwa na uhaba wa watumishi kwani wapo 47 kati ya 200 wanaohitajika.

Mbunge wa Handeni Vijijini, John Sallu ameomba Serikali isaidie kupatikana gari la wagonjwa hospitalini hapo kwani inapokea wagonjwa wengi wa dharula lakini pia kijengwe chumba maalum kwa wagonjwa wa mifupa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live