Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imezindua magari ya "Kliniki Tembezi" kwaajili ya kupima TB

MAABARA GARI Serikali imezindua magari ya "Kliniki Tembezi" kwaajili ya kupima TB

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo September 6, 2021, Wizara ya Afya nchini imezindua magari yenye maabara za kisasa kwaajili upimaji na mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu. Magaro hayo yatapelekwa kwenye maeneo ya vijijini ambako kuna changamoto za maabara, uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Tiba na Kinga, Dr. Leonard Subi imeeleza kuwa Magari hayo yamesheheni vipimo vya kisasa vya kupimia kifua kikuu, ikiwemo X-Ray, na mashine ya vinasaba pamoja na mashine ya upimaji moyo. Kupitia kliniki tembezi wananchi wataweza kupima ugonjwa wa kifua kikuu na kupata majibu ndani ya masaa mawili, ambapo hapo awali upimaji wa ugonjwa huo majibu yalikuwa yakitoka baada ya siku mbili.

"Magari hayo ni yakisasa na yatakuwepo kila kanda, ikiwemo kanda kati, kanda ya mashariki , kanda ya nyanda za juu kusini pamoja na kanda ya kaskazini nia ni wakuwafikia wananchi yatapita kwenye mitaaa ,hasa vijijini na sehemu ambazo huduma ya afya hazifiki vizuri."

" Hata hivyo, kuna wataalamu wazuri sana afya kwenye gari hayo na yatasaidia kugundua watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kifua Kikuu ikiwa ni asilimia 63% ya walioathirika na 37% hawajagunddulika na ifahamike kuwa huduma za ugonjwa huo ni bure." - Dr. Subi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live