Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imeanza kuajiri Watumishi sekta ya afya – Dkt. Mwinyi

Sad Afya Serikali imeanza kuajiri Watumishi sekta ya afya – Dkt. Mwinyi

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kuajiri Wauguzi na imeongeza nafasi za ajira kwa madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Mei 12, 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Polisi aliyewauwa wageni wawili, kujeruhi auawa Amesema, Serikali imefanya jitihada kubwa kwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya, kujenga miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali za Wilaya na Mkoa pamoja na vituo vya afya Unguja na Pemba.

Aidha, Rais Mwinyi pia amesema Serikali imeendelea na juhudi za ununuzi wa vifaa vya tiba na uchunguzi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live