Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Watanzania hawatafungiwa ndani, anayetaka ajifungie

9c09e0f888d9dbb1e6a1eb2740c5ef40 Serikali: Watanzania hawatafungiwa ndani, anayetaka ajifungie

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imeendelea kusisitiza kuwa haitawafungia Watanzania na badala yake imewataka kuchukua tahadhari ya kujikinga bila ya kutishwa au kuchomekewa mawazo na mikakati na watu wengine katika mapambano dhidi ya UVIKO -19 (Covid 19).

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi wakati akizungumza na waandishi jijini Dodoma.

Amesema mwongozo wa Serikali kuhusu kile kinachoendelea duniani kuhusu ugonjwa wa mlipuko wa Corona ni kuendelea kuchukua tahadhari kama ilivyotamkwa na Rais, John Magufuli katika ziara yake Kanda ya Ziwa wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Rais Magufuli akiwa Kanda ya Ziwa aliwataka wananchi kuchukua taadhari za ugonjwa wa Corona ikiwemo mazoezi huku akisisitiza watu kujikita katika shughuli za kiuchumi kama kilimo ikiwemo kulima sana.

Kifupi cha ugonjwa wa virusi vya corona ni UVIKO - 19 ndiyo Kiswahili sanifu, Rais amesisitiza duniani ugonjwa unaendelea na kwa sababu ya mwingiliano baina yetu na nchi nyingine ni lazima tuendelee kuchukua tahadhari.

“Watanzania waendelee kuchukua tahadhari zote lakini tusiwe na woga wala tusichomekewe mawazo na mikakati ya watu wengine,” amesisitiza.

Chanzo: habarileo.co.tz