Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Rufaa za Lindi kuhudumiwa Lindi

Dkt Mollel Azitaka Taasisi Za Afya Kuwasaidia Wafanyabiashara Serikali: Rufaa za Lindi kuhudumiwa Lindi

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Kesho anataraijiwa kuzindua hospitali ya mkoa huo.

Hospitali hiyo inatajwa kuwa na vifaa vya kisasa kama vile mashine ya kugeuza kitanda cha mgonjwa kwa kutumia [remote control] na mashine inayotumia teknolojia ya Akili Mnembe [ Artificial Intelligence] itakayotumika kuchunguza saratani ya matiti.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akiwasalimia Wananchi wa Mtama mkoani Lindi wakati wa ziara ya Rais Samia ikiendelea mkoani humo.

Ameongeza kuwa hospitali hiyo itatumika kuhudumia rufaa zilizokuwa zikipelekwa Dar es Salaam.

Baada ya kuzinduliwa, hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Lindi itaanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje, huduma za wagonjwa wa dharura, huduma za Radiolojia na itamaliza Rufaa zote za huduma za CT Scan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live