Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema Wizara imejiwekea malengo ya Miaka mitano (2020-2025) ya kusomesha wataalamu Bingwa na Wabobezi wasiopungua 300 kila Mwaka, kwa Mwaka 2020/21 na 2021/22 wamesomesha wataalamu Bingwa 524 ambao wanaendelea na masomo ndani na nje ya nchi.
Amesema “Hadi Desemba 2021 tulibaini mahitaji ya Madaktari Bingwa katika Hospitali za Serikali zinazotoa huduma za kibingwa na kibobezi ni 1,782 wakati Wataalamu waliosomeshwa na Serikali ni 992”.
Serikali inakuja na utaratibu wa kutoa ufadhili kwa Wataalamu hao wa Afya kwa Utaratibu wa seti ili kuimarisha Huduma ya matibabu na kupunguza rufaa za nje ya nchi.