Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali Kigoma yajpanga kukabiliana na magonjwa ya moyo

Serikali Kigoma Yajpanga Kukabiliana Na Magonjwa Ya Moyo Serikali Kigoma yajpanga kukabiliana na magonjwa ya moyo

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali mkoani Kigoma imesema inajipanga kuimarisha huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kigoma ili waweze kuanza kutoa huduma za matibabu ya awali ya moyo baada ya kuongezaka kwa kiasi kikubwa cha wananchi wanaohitaji huduma hiyo. - Katibu Tawala Mkoa Kigoma, Hassan Rugwa amesema hayo wakati wa kuhitimishwa kwa kliniki ya matibabu ya upimaji na matibabu ya awali ya magonjwa ya moyo kliniki iliyokuwa ikiendeshwa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). - Rugwa amesema kuwa kambi hiyo ya madaktari bingwa imeonyesha uhitaji mkubwa wa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa Kigoma hivyo wanajiandaa kuhakikisha upimaji wa awali na matibabu ya awali yanafanyika wakati wote sambamba na kuandaa kambi za madaktari bingwa mara nyingi. - Akizungumza mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Eva Wakuganda amesema katika siku tatu za huduma ya kambi hiyo wameona watu 351 ambapo kati yao watu 19 walikutwa na matatizo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI. - Dk Wakuganda amesema kwa upande wa wagonjwa waliopewa rufaa ambao watu wazima walikuwa 11 walikutwa na matatizo mbalimbali ya moyo ikiwa ni pamoja na kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo, kutanuka kwa moyo, shida za valvu na mfumo wa umeme wa moyo kutokufanya kazi vizuri. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live