Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seli za Ubongo zilotengenezwa maabara zinacheza Ping Pong

WhatsApp Image 2022 10 13 At 1.jpeg Seli za Ubongo zilotengenezwa maabara zinacheza Ping Pong

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasayansi wamezifunza seli za ubongo kucheza mchezo uitwao ping pong ambapo wachezaji wawili hutumia kasia kuupiga mpira mbele na nyuma na huishia kutengeza mlio wa pong na ndio maana kuishia kuitwa pong, ikiwa seli laki nane zimefuzu mchezo huo uliotengenezwa mwaka 1972, seli hizi zinakuwa kwenye kisahani kilichozungushiwa na elektroni ambazo husaidia katika shughuli za ubongo kufanya kazi.

Kampuni kama Google ina mashine inayotumia akili bandia (Artificial intelligence) na imeshachezeshwa mchezo wa Pong na kufanikiwa kuuweza, hizo seli za ubongo zinazocheza mchezo haziitikii kwa ishara ya kuona bali ni kwa ishara ya elektroni za umeme.

Afisa mwanasayansi mkuu katika maabara ya Cortical iliyotengeneza seli hizo za ubongo kuwa na uwezo wa kucheza mchezo wa pong amesema:

”Kwenye vitabu vya sasa, niuroni zimefikiriwa haswa kuwa kwa maana ya biolojia ya mwanadamu ana ya wanyama, Hazifikiriki kama mchakataji wa habari lakinj niuroni ni mfumo mzuri sana unaoweza kuchakatua habari kwenye hali halisi na pia kwa kutumia umeme mdogo sana”

Kazi hiyo ya kutengeneza seli zichezao mchezo haifanyiki kama kitu cha kujifurahisha tu bali inalenga katika majaribio  kama vile kupima uwezo wa madawa ya kulevya mapya na madhara yake kwenye ufanyaji kazi wa niuroni za ubongo, mwanasayansi wa niuroni Takuya Isomura anayefanya kazi katika kituo cha sayansi ya Ubongo huko Saitama, Japan, amesema kuwa haijawa wazi kama seli hizo zilikuwa zinaonesha tabia hizo ili zijitengenezee mazingira ya kutabilika ama tu kwa muitiko wa vingele vya ishara ambazo inapokea.

Kampuni hio ya Cortical imeipa jina mfumo huo jina la ubongo wa sahani ingawa Kagan amesema kuwa  niuroni hizo ni kilio cha mbali sana kuanza kuziita ubongo halisia mapema hivi, ubongo wa sahani ni modeli nzuri ya ubongo itakayoruhusu kufanya majaribio kwa mapembejeo tofauti kagan amesema:

”Tunajaribu kutengenza dozi ya ethanol, tuzileweshe tuone kama zitacheza mchezo huo vibaya, kama ambavyo watu wakinywa huwa.”

Mhandisi wa niuroni Steve Potter ambaye yeye ikiwemo na kikundi chake mwaka 2008, walitoa taarifa kuwa niuroni zilochukuliwa kutoka kwa panya zilionesha kujifunza na tabia ya kufwata malengo, kampuni ya maabara ya Cortical ambayo kwa sasa inafwata kazi ya mhandisi wa niuroni Potter, Steve Potter na wenzie walifanya majaribio hayo kwa seli za panya tu lakini kikundi cha maabara ya Cortical kimejaribu kupima na niuroni zilizotokana na seli za mwanadamu.

Maabara ya Cortical imelenga pia kutumia niuroni kutengeneza kitengo cha usindikaji wa ki biolojia kwa kiweza kutumika kwenye kompyuta na mbinu zilizotengenzwa katika mfumo huo zinawdza kutumika kupima uwezo wa kujifunza na uelewa kwa wanyama na wanadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live