Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya afya kuendelea kuboreshwa

Serikali Itaendelea Kuwekeza Kwenye Vyanzo Vya Uzalishaji Wa Gesi   Majaliwa Sekta ya afya kuendelea kuboreshwa

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kuboresha sekta ya afya ili kusogeza huduma bora za afya karibu na Wananchi.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa hospitali ya wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Majaliwa ameagiza kuendelea kukamilishwa kwa ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na kununua vifaa tiba ili kuimarisha hali ya utoaji huduma kwa Wananchi.

“Kukamilika kwa hospitali hii kutasaidia kupunguza gharama kwa wakazi wa maeneo ya karibu kutembea umbali mrefu hadi Tarime kufuata huduma za afya, hospitali hii ni suluhisho,' amesema Waziri Mkuu.

Ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya ya Rorya umeishatumia shilingi Bilioni 3.25 ambapo kwa sasa inahudumia takribani wagonjwa 400 kwa mwezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live