Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saratani ya macho tishio kwa watoto

58254 Pic+macho

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya kuwa ni ugonjwa usiofahamika sana katika jamii, saratani ya macho kwa watoto inatajwa kuwa miongoni mwa magonjwa tishio.

Wastani wa watoto 60 hadi 80 kwa mwaka hufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya tatizo hilo linalosababisha upofu na vifo.

Wakati hali ikiwa hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa katika kila mwaka, wastani wa watoto 100 hadi 130 hukumbwa na ugonjwa huo.

Hayo yaliezwa jana na daktari bingwa wa macho, Anna Sanyiwa wakati wa uchunguzi wa saratani ya macho kwa watoto, uliofanyika Hospitali ya Mloganzila ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya kimataifa ya saratani ya macho kwa watoto.

Alisema tatizo hilo ni kubwa tofauti na wengi wanavyodhania na linakua kwa sababu watoto wengi hufikishwa hospitali wakiwa kwenye hatua mbaya.

Dk Sanyiwa alisema kwa hospitali ya MNH, aina hiyo ya saratani ni ya pili kwa kuwa na wagonjwa wengi waliopo wodini.

Pia Soma

“Huu ugonjwa upo na unatibika ukiwahi mapema hospitali. Tatizo wengi wanaletwa wakiwa tayari wameathirika vibaya na ikifika hatua hiyo, ni ngumu kuitibu,” alisema.

Dk Sanyiwa alisema ni muhimu kwa wazazi kuwachunguza watoto wao na kuwafikisha mapema hospitali wanapoona tofauti.

“Ukiona mtoto ana kengeza au weupe kwenye jicho, usione ni kitu cha kawaida mpeleke hospitali akafanyiwe uchunguzi. Ukiwahi kupata matibabu katika hatua za awali anapona kabisa, ukimchelewesha jicho linaharibika na inaweza kusababisha hadi kifo.

Leila Mapenzi, mmoja wa watu waliojitokeza kupeleka watoto wao kufanyiwa uchunguzi jana, aliliambia Mwananchi kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona dalili za hali tofauti kwenye macho ya mtoto wake.

“Nimesikia taarifa kuhusu saratani hii, nikaona nimlete afanyiwe uchunguzi maana anajikuna sana kwenye macho yake,” alisema mzazi huyo.

“Tatizo hili tatizo limeanza tangu akiwa na miezi sita sasa ana miaka mitatu.”

Chanzo: mwananchi.co.tz