Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia akiri Omicron ipo nchini

3aa059f28f3cec4c37e903f061e4dcac Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amehutubi Taifa leo Ijumaa kuelekea Mwaka Mpya 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam na haya hapa ni baadhi ya mambo muhimu aliyoyagusia.

Janga la UVIKO-19

Kwamba tayari wimbi la nne la maambukizi ya UVIKO-19 yanayotokana na kirusi cha omicron kimesha ingia nchini na kuathiri idada ya Watanzania. Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote muhimu.

Mfumuko wa bei

Mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini ya asilimia 5 na mwaka 2021 ulifikia asilimia 4.1. Kiwango cha mfumuko wa bei kilichochewa na janga la UVIKO-19 na kupanda bei ya bidhaa za petroli kwenye soko la kimataifa. Hata hivyo, utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na IMF ya Sh trilioni 1.3 pia ulipandisha bei ya vifaa vya ujenzi katika soko la ndani.

Amani na Usalama

Nchi inaendelea kudumisha amani na maelewano. Nawashukuru Watanzania kwa kudumisha amani na mshikamano.

Fedha za kigeni

Hivi sasa, nchi inazaidi ya dola za kimarekani bilioni 6.25.

Sensa

Mwaka 2022 ni mwaka wa sensa ya watu kitaifa na naomba kila mtu ashiriki ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi.

Utalii

Rais Samia alikiri kwamba sekta ya utalii iliathiriwa vibaya na janga la UVIKO-19 ambalo sasa liko kwenye wimbi lake la nne. Hata hivyo, alitangaza kuwa idadi ya watalii wanaowasili nchini iliongezeka kwa watalii 779,133 hadi kufikia milioni 1.400 mwaka 2021.

Biashara na Mahusiano

Serikali ilifanya marekebisho katika sera zake na mfumo wa kikodi ambayo pia iliongeza kiwango cha uwekezaji kutoka miradi 186 mwaka uliotangulia hadi biashara 237 mwaka 2021 ambazo zilikuwa na thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 414.

Kilimo

Mapema wakani wakulima watapata mbolea ya kukuzia ambayo ni sawa na bei iliyozoeleka hata hivyo uwekezaji unaofanyika Dodoma utaongeza upatikanaji wa mbolea. Mfanyabiashara Alko Dangote pia ameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha mbolea huko Mtwara

Chanzo: www.tanzaniaweb.live