Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia Suluhu atokwa machozi uzinduzi kampeni ya afya ya uzazi

25731 Makamu+pic TanzaniaWeb

Wed, 7 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma/Dar. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametokwa na machozi wakati wa igizo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga nchini.

Samia alitokwa na machozi leo jijini Dodoma wakati kikundi cha maigizo na bendi cha Mrisho Mpoto kilipokuwa kikionyesha igizo maalum kuhusu afya ya uzazi.

Kwa kipindi chote cha igizo hilo Makamu wa Rais alionekana akihuzunika na baadaye mwanamke aliyeigiza mjamzito alipolia kupoteza mtoto wake, alivua miwani na kuinama kwa muda mrefu kisha alifuta machozi machoni mwake..

Madhumuni ya kampeni hiyo ni kuhamasisha viongozi wa Serikali, dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, watoa huduma za afya, familia na jamii kwa ujumla kuchangia juhudi za taifa za kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na vya watoto wachanga.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge alisema kujengwa kwa vituo vya afya  21 mkoani Dodoma kumechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuwafikia wanawake wengi zaidi.

“Tunamshukuru waziri wa afya na timu yako kwa jinsi mnavyofanyakazi lakini na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla, tumetoka kwenye bajeti ya Sh900 fedha za dawa na sasa tunapewa zaidi ya Sh4 bilioni,” alisema.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Chanzo: mwananchi.co.tz