Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za maumivu ya nyayo kwa wakimbiaji

17786 Shita+Samweli TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika maisha ya mwanamichezo mkimbiaji ni kawaida kuwahi kukabiliwa na maumivu ya chini ya mguu katika mbonyeo wa nyayo.

Inawezekana pia Mwanariadha mstaafu wa mbio ndefu kimataifa Mzee Akwari kuwa na uzoefu na tatizo hili katika enzi za maisha yake ya ukimbiaji.

Tatizo hili hujulikana kitabibu kama plantar fasciitis au runner’s heel mara kwa mara huwapata wakimbiaji na kuwasababishia maumivu chini ya nyayo yanayochoma kama kitu chenye ncha kali.

Tatizo hilo hutokea baada ya kuwepo kwa shambulizi ndani ya nyayo kwenye bunda gumu la tishu iliyojitandika kama kitambaa kigumu na kuunganisha mfupa wa kisigino na dole gumba la mguu.

Baadhi ya watu hudhani pengine tatizo hili linawapata zaidi wakimbiaji wa mara ya kwanza au wenye uzito mkubwa lakini kumbe yoyote anayefanya zoezi la kukimbia anaweza kupata.

Karibu asilimia 10 hadi 20 ya wanariadha duniani inasemekana wamewahi kupata tatizo hili katika maisha yao na zaidi kwa wale wakimbiaji wenye umri wa zaidi ya miaka 35-40.

Wanariadha, umri mkubwa, uzito mkubwa, uvaaji viatu vigumu na soli ndefu, dosari ya kuzaliwa ya unyayo, aina ya mchezo na kazi ni sababu ya kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili.

Wakimbiaji ambao ni wafanyakazi wa viwandani, walimu, wachuuzi wakutembeza bidhaa na askari ni makundi ya jamii ambayo aina ya kazi yao inawahatarisha kupata tatizo hili.

Dalili kubwa ni maumivu ya kuchoma katika eneo la kisigino na mbonyeo wa nyayo mara tu unapoamka asubuhi na kuanza kupiga hatua chache.

Baada ya hatua kuchanganya na unaposimama maumivu yanaweza kupotea kwa dakika kadhaa, huanza tena mara tu unapoanza kutembea tena.

Sababu ya maumivu haya kujitokeza asubuhi baada ya kuamka ni kutokana na tando ngumu ya nyayo wakati wa usiku huwa imesinyaa na kuwa ngumu hivyo unapoikanyagia ghafla nyuzi zake huvutika.

Kwa kawaida nyayo hufunikiwa na ngozi na kufuatiwa na tando ngumu ya tishu inayoshikamana na misuli, tando hii ndiyo inayoaminika kuathirika na kusababisha maumivu.

Kama ilivyo maeneo mengine ya mwili eneo hili ndani yake huwa na tishu zingine ikiwamo mishipa ya damu na ya fahamu, hivyo tishu hizi pia huweza kupata majeraha na kuongeza ukubwa wa tatizo.

Wakati wa kukimbia huwepo mgandamizo mkubwa wa uzito mwili katika nyayo, kulika na kuchanika kwa tishu za tando ngumu ya nyayoni husababisha mkereketo unaoleta maumivu.

Mara kadhaa tatizo hili huwapata wenye uzito mkubwa na sababu kubwa ni miguu inapotua chini hupata mgandamizo mkubwa na kupondwa na mfupa uliobeba mwil na matokeo yake huziponda nyama na kusababisha kupasuka.

Pamoja na tatizo hili kumstua muathirika kutokana na maumivu ya kukera linaweza kuondoka lenyewe bila matibabu yoyote. Wakati mwingine ni mtawanyiko wa tishu zenyewe na kwa kuwa unapokimbia ni kama inahama kwenye mgandamizo mkali na baadaye zinarudi na hapo ndipo kuna maumivu.

Tukutane Jumatatu ijayo nitaeleza njia salama za kulikabili tatizo hili.

Chanzo: mwananchi.co.tz