Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za kuzaa watoto wenye mtindo wa ubongo zatajwa

78619 Pic+mhagama

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upungufu wa madini ya chuma mwilini, viini lishe, ulevi uliopindukia, ugomvi uliokithiri wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa bila maelekezo ya daktari kujifungua katika maeneo yasiyo salama zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia watoto kuzaliwa na utindio wa ubongo.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Buge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati wa maadhimisho ya siku ya utindio wa ubongo yanayofanyika kila Oktoba.

Akizungumza wakati wa kufungua maadhimisho hayo, Waziri Mhagama amesema anatambua changamoto wanazokutana nazo walezi na wazazi wa watoto hao huku akitoa wito kuzingatia vitu ambavyo vinaweza kupunguza uwezekano wa kupata watoto walio na matatizo hayo.

“Naomba nitoe wito kwa kina mama kuepuka haya yote ili kupata watoto walio salama na wazazi wa kiume waache kuwasumbua na kuwanyanyasa wakina mama wanapokuwa wajawazito kwa sababu inaweza kufanya mama ajifungue mtoto aliye na matatizo ya utindio wa ubongo.”

Pia, amewataka wazazi walio na watoto hao kuwalea vizuri na kuhakikisha wanapata fursa ya elimu, huduma za afya pamoja na kuhifadhiwa kama watoto wengine.

“Wazazi walio na watoto wenye tatizo la utindio wa ubongo, wasijinyanyase na kunyanyasa watoto wasiwafungie ndani bali wawatoe na kuwaleta huku ili waweze kupata fursa kama ilivyo kwa watu wengine,” amesema Mhagama

Pia Soma

Advertisement
Awali, katibu wa chama cha wazazi wa watoto walio na ulemavu wa mtindio wa ubongo, akili na viungo Tanzania (Chamaumavita) Mwanahamisi Hussein amesema malezi kwa watoto hao imekuwa ni changamoto kwa wazazi wengi jambo ambalo linahitaji usaidizi.

“Ndiyo maana tuliwaandalia majukwaa kama haya ili kuwasaidia wao waondokane na upweke wakutane na wenzao, wabadilishane mawazo na kushirikishana changamoto zao ili waweze kuwa na sauti za pamoja,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz