Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya watoto kutoathirika na COVID-19

Chanjo Ya Mtotoo Chanjo

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MGANGA Mkuu wa Hospitali ya Rufani ya Mount Meru mkoani Arusha, Dk. Sunday Wanyika, amesema kuwa kufa na kuzaliwa kwa seli mara kwa mara katika miili ya watoto ndiyo sababu inayowakinga kutoshambuliwa na virusi vya corona.

Aliyasema hayo jijini Arusha wakati akitoa mada kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa corona kwenywe mkutano wa wadau kuhusu masuala ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki kwa wananchi katika kipindi cha matumizi ya lugha ya kiswahili.

Mganga huyo alisema hali hiyo ndiyo imekuwa ikisababisha watoto kutoshambuliwa na virusi hivyo, kwani vinapotaka kushambulia vinakuta seli zimekufa na kuanza kuzalishwa nyingine.

"Zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa hawaonyeshi dalili na wanaongoza kwa kusambaza virusi vya ugonjwa huo, hivyo wakati wa kujikinga usiwahofie ambao wameshaugua na kuonyesha dalili tu, muwe makini pia na kundi hilo, mpaka sasa watu milioni 199 wameshapimwa na kukutwa na maambukizi huku watu milioni nne wakifariki na ugonjwa huo ulimwenguni,”amesema Dk. Wanyika.

Alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa makini kwa kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo kwa kuchukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanachoma chanjo ambalo ni lazima kutokana na hali halisi ilivyo sasa, kutokwenda kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima na kutulia majumbani, kuvaa barakoa ambazo zinakinga, kutumia vitakasa mikono na kunawa maji tiririka.

Kuhusu virusi vya corona awamu ya tatu, Dk. Wanyika alisema viko tofauti na vile vya awamu ya kwanza, husambaa kwa haraka zaidi na ni rahisi kusababisha kifo, huku akitaja dalili namba moja kuwa ni kifua kuuma na kuwa kizito wakati awali ilikuwa ni kupata mafua, kukohoa na kushindwa kunusa.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Godfrey Pinda aliwataka mawakala wa sheria kwenye maeneo yao wapambanie afya za watu wao suala la chanjo ni muhimu sana kwa maisha ya Watanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live