Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Waziri kuagiza Daktari aliyetetemeka asirekodiwe

Dkt Na DKT CHIZ Sababu ya Waziri kuagiza Daktari aliyetetemeka asirekodiwe

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale, amesema kuwa sauti ya Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, iliyosikika ikitoa maelekezo kuwa Daktari aliyetetemeka wakati wa mdahalo wa COVID-19 asirekodiwe ni kutokana na maadili ya kazi na ufaragha wa mgonjwa.

Juzi Agosti 12, 2021, wakati mdahalo huo ukiendelea Dkt. Sospeter Bulugu, alishindwa kuwasilisha mada yake baada ya kupata kizunguzungu kilichotokana na sukari kwenye damu kushuka, na kwamba Watanzania wametakiwa kupuuza uzushi huo kuwa alitetemeka kutokana na madhara ya chanjo ya COVID-19.

Aidha, Dkt. Sichwale ameeleza kuwa madai ya kuwa Waziri wa Afya, alitaka kuficha jambo kuhusu madhara ya chanjo si ya kweli kwani kuvitaka vyombo vya habari visichukue tukio hilo yeye alikuwa akitekeleza majukumu yake ya maadili ya kitaaluma pale panapokuwa na mteja anayepokea huduma ambaye hajaridhia kwa hiari yake kwamba huduma hiyo iwe wazi.

Dkt. Sichwale ameongeza kuwa hata hivyo Dkt. Bulugu aliyekutwa na changamoto hiyo hajawahi kupata chanjo ya COVID-19.

Chanzo: eatv.tv