Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu wenye kisukari kupata kiharusi

Diabetes Injection Sababu wenye kisukari kupata kiharusi

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Hutokea mara nyingi wagonjwa wa kisukari acha aina ya pili hupata changamoto ya kuugua kiharusi.

Tatizo hili mara nyingi huwaacha wakiwa na ulemavu wa kudumu kutokana na kupooza.

Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa watu wenye kisukari huwa katika hatari ya kupata kiharusi mara 1.5 ukilinganisha na wasiokuwa nacho.

Kisukari kisichodhibitiwa huathiri uwezo wa mwili kutumia kichochezi cha Insulini kwa ufanisi ikiwamo utengenezwaji na matumizi yake.

Kichochezi hiki ndicho huelekeza seli kutumia sukari (glucose).

Pale kiwango cha sukari kikiendelea kuwa juu kwa muda mrefu ndipo husababisha mishipa ya fahamu na damu kuharibika.

Kiharusi hutokea pale tishu za ubongo zinapokosa damu aidha kwa muda tu au kudumu kutokana na kizuizi au kunyauka na kuwa myembamba.

Pia iwapo mishipa itapasuka na hivyo kupeleka damu chache katika ubongo au kutopeleka kabisa.

Na hii ndiyo sababu wanasayansi wa tiba wanalianisha tatizo hili kama kiharusi ambacho huwa ni la muda tu kutokana na mshipa unaopeleka damu yenye oksijeni kuzuiwa na kimgando au kibuja.

Aina ya pili inatokana na mishipa ya damu kupasuka au kuvujisha damu aidha ni baada kuharibika au pale msukumo mkubwa unapotokea husababisha kupasuka na kuvujisha damu katika ubongo.

Aina hii ya kiharusi huwa na matokea mabaya ikiwamo kuchangia kupooza kwa kudumu katika baadhi ya sehemu za mwili au mwili mzima.

Aina ya tatu huwa ni upelekwaji wa damu katika ubongo kuzuiwa kwa muda mfupi tu na huwa hakuna kuambatana na matatizo ya kudumu ya majeraha ya mfumo wa fahamu.

Aina ya kwanza husababisha tatizo la muda tu, pale kizuizi kinapoondoka hali ya kupooza au athari katika kiungo fulani hutoweka.

Hapa mgonjwa anaweza kuwa na viashiria kama kupinda kwa mdomo, udhaifu wa mikono na kushindwa kuongea.

Baada ya msukumo wa juu wa damu kudhibitiwa au kizuizi kuondolewa au kutoweka dalili hizi hutoweka.

Wakati kwa kiharusi cha aina ya pili ambacho damu huvuja katika ubongo husababisha tishu za eneo hilo kukosa lishe kwa muda mrefu, hivyo kuchangia ulemavu wa kudumu.

Sababu kubwa ya wagonjwa kupata tatizo hili kirahisi kwa wagonjwa wa kisukari ni kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika damu, hatimaye husababisha kurundikana kwa mafuta kwenye mishipa ya damu.

Hali hii husababisha vimgando vinavyosababisha mishipa kuwa myembamba au kuweka kizuia katika mishipa ya damu ya ubongo au shingoni.

Matokeo yake husababisha kuzuia kwa damu kwenda katika ubongo hivyo tishu hizo hukosa damu yenye hewa ya oksijeni na hatimaye kiharusi hutokea.

Ukubwa wa kiharusi na athari zake itategemeana na eneo lililokosa damu, aina ya mshipa wa damu ulioathirika, muda na vihatarishi mbalimbali.

Ili kupunguza hatari ya kupata kisukari na kiharusi dhibiti ulaji holela wa vyakula kama sukari, mafuta na chumvi.

Kula zaidi lishe ikiwamo mlo wenye samaki, mboga mboga, maharage na jamii ya karanga.

Fanya mazoezi kwa siku dakika 30 mpaka 60 kwa siku tano za wiki, epuka matumizi ya tumbaku na ulevi wa pombe na shikamana na matibabu.

Chanzo: mwananchidigital