Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu tatu za Askofu Bagonza kupata Chanjo

BAGONZA Askofu Bagonza akipata Chanjo

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: Mwanahalisi

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Dayosisi ya Karagwe Mkoa wa Kagera,Dk Benson Bagonza ametoa sababu kuu tatu zilizomsukuma kujitokeza na kupata Chanjo ya Corona.

Dk Bagonza ametoa sababu hizo leo Ijumaa Agost 6,2021 mara baada ya kukamilisha zoezi la kuchoma Chanjo hiyo katika Hospitali teule ya Wilaya ya Karagwe.

Akifafanua sababu hizo kuu tatu,Dk.Bagonza amebainisha kuwa amefanya tafiti kwa madaktari wetu hapa nchini,USA,Ulaya na Canada.Nimeridhika na maelezo waliyonipa.

Pili,vita ya Kibiashara kwa Makampuni makubwa ni ya muda wote kwa bidhaa zote. Wanaokuuzia T-shirt ya kuzuia risasi,kesho wanatengeneza risasi ya kupenya kwenye T-shirt waliyokuuzia jana.

Akielezea sababu ya tatu,Askofu Bagonza amesema Chanjo ya Jensen inazuia kupata Corona,Chanjo hii inazuia kwa asilimia 86 usiingie katika ugonjwa mkali.Na chanjo hii inazuia kifo cha Corona kwa asilimia 100.

Mimi nimeridhika. Una hiari ya kuamua unavyopenda, Nimewahi kuugua Corona kwenye wimbi la kwanza na nimezika wengI. Ratiba yangu imejaa kwa wiki nzima mbele kwa ajili ya mazishi.Nimechagua kufa kesho siyo leo"amesisitiza Askofu Bagonza.

Chanzo: Mwanahalisi