Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu kuzaliwa watoto njiti Chamwino zatajwa

30050c5d798e1357ea6f54d814a26607 Sababu kuzaliwa watoto njiti Chamwino zatajwa

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

ONGEZEKO la mimba za utotoni katika wilaya ya Chamwino limetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa watoto wengi njiti katika wilaya hiyo.

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga wakati akipokea vifaa tiba kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) vyenye thamani ya Sh milioni 25 kutoka Taasisi ya Doris Mollel Foundation.

Alisema kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa wataunda kampeni maalum ili kupunguza changamoto ya kuzaliwa watoto njiti.

Awali, akisoma taarifa ya huduma za afya wilaya ya Chamwino, mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wilayani hapa, Neema Mlula alisema upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya afya ni wa kuridhisha kwani kwa mwaka 2020 kulikuwa na asilimia 87.5 ya upatikanaji wa dawa, lakini kwa kipindi cha robo ya tatu Oktoba hadi Desemba, mwaka jana upatikanaji wa dawa muhimu ulikuwa ni asilimia 83.5 na hiyo ni kutokana ukosefu wa dawa kwenye Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Dk Venus Mgaiga alisema pamoja na mafanikio yaliyopo lakini kuna changamoto katika hospitali hiyo ikiwamo upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel alisema natoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu yenyewe.

Mwenyiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani humo, Neema Majule aliipongeza taasisi hiyo kwa kutoa vifaa hivyo akisema vitasiaida kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa huduma bora za afya na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kuvitunza vizuri.

Mama wa mtoto njiti anayefahamika kwa jina la Jemima Madonna alisema kuna changamoto kubwa ya kulea waoto hao na kuishukuru taasisi hiyo kwa kutoa vifaa hivyo na kuiomba serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili.

Chanzo: habarileo.co.tz