Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu kubugia ARV bila kupima hizi hapa

39519 Arvpic Sababu kubugia ARV bila kupima hizi hapa

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Imeelezwa kuwa watu wengi wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanatumia dawa za kufubaza Ukimwi (ARV), lakini hawako tayari kuweka wazi taarifa zao kwa sababu ya unyanyapaa.

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids) Dk Leonard Ma­­­­boko ameeleza hayo leo Ijumaa Februari Mosi wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Amesema waathirika wengi wanaogopa kusema ukweli hata pale wanapoulizwa na wataalamu au watafiti.

"Baadhi ya watu wakihojiwa wanasema hawajawahi kupima wala hawajui kuhusu afya zao, lakini damu zao zikipimwa zinagundulika kuwa tayari wanatukia dawa za kufubaza Ukimwi (ARV)," amesema.

Dk Ma­­­­boko  amesema kitendo cha watu kutoweza kuweka bayana hali zao licha ya kutumia ARV ni ishara kuwa kuna unyanyapaa katika jamii.

Juzi, Dk Maboko alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema Watanzania wengi wana mwamko wa kutumia ARV  kuliko kujua hali zao.

 Alibainisha hayo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano wa taasisi ya kupambana na maambukizi ya VVU ya AGPAHI.

 "Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 90 wanawake wajawazito wanajua hali zao na kati yao asilimia 98 wanatumia dawa za ARV. Hata hivyo, katika utafiti uliofanyika ilibainika kuna watu hawajui hali zao lakini walipopimwa damu zao zilionyesha kuwa tayari wanatumia ARV," alisema Dk Maboko.



Chanzo: mwananchi.co.tz