Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu, dalili na matibabu ya kiharusi

Kiharusi Kiharusiiii.jpeg Sababu, dalili na matibabu ya kiharusi

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiharusi ni hali ya kuziba (ischemic) au kupasuka (hemorrhagic) kwa mishipa ya damu ya ubongo na kisha kupelekea ku ‘paralize’ au kifo. Kuna wakati ububu, uziwi, upofu hutokana na kiharusi.

Asilimia 85 ya kiharusi (ischemic stroke) hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu. Licha ya kutokea kwa asilimia 15 aina ya pili, yaani hemorrhagic stroke ni mbaya sana na mara nyingi hupelekea kifo.

VIHATARISHI VYAKE

Kiharusi kinaweza kumpata mtu yeyote yule lakini wafuatao wana uwezekano Zaidi wa kupata kiharusi.

◉ Mwenye umri Zaidi ya miaka 55

◉ Mwenye historia ya kiharusi kwenye familia yake

◉ Mwenye kisukari ambacho hakijathibitiwa

◉ Mwenye shinikizo la damu (BP) ambayo halijathibitiwa

◉ Mwenye maradhi ya mishipa ya damu ya ubongo

◉ Mwenye maradhi ya moyo

◉ Mwenye maradhi ya kukosa usingizi

◉ Mwenye cholesterol nyingi, mnene wa kupindukia, Kutofanya mazoezi

◉ Uvutaji wa sigara

◉ Unywaji pombe

◉ Utumiaji wa madawa ya kulevya.

DALILI ZAKE

◉ Kushindwa kuongea au kutamka maneno sawasawa

◉ Kupinda uso na kushindwa kutumia mkono ama mguu

◉ Kizunguzungu na kukosa balance

◉ Kutokuona vizuri

◉ Kichwa kuuma.

MATIBABU YAKE

Kuwahi haraka hospitali ndani ya saa 24 ili kupewa dawa ya kushusha shinikizo la damu na ubongo na kuzuiza kifafa kisha kufanya vipimo vya kichwa yaani CT scan au MRI, na ultrasound.

Madaktari na wauguzi watakushauri kuhusu kuanza matibabu ya haraka ya kuzibua mishipa ya damu (Angiosuite) au kuondoa donge la damu kwa upasuaji (Theathre).

Baada ya kudhibiti hali ya dharura, utashauriwa kuanza mazoezi tiba (physiotherapy) pamoja na kuwaona jopo maalum la madaktari wa kiharusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live