Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SMZ yaomba taasisi kuwasaidia wagonjwa huduma ya matibabu

11131 SMZ+PIC.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed amezitaka taasisi zinazoendesha uchunguzi wa magonjwa kutoiachia Serikali mzigo wa matibabu baada ya kuwabaini wenye kuhitaji matibabu.

Akizungumza jana na uongozi wa taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (Jai) ambayo inatarajia kufanya uchunguzi wa afya kwa wananchi Agosti mwaka huu

Hamad alisema taasisi hiyo inapaswa kuwapatia matibabu wananchi watakaobainika kuwa na maradhi mbalimbali.

Alisema zipo baadhi ya taasisi hufanya kazi ya kuchunguza afya za wananchi na kubaini maradhi yanayowakabili, lakini zinashindwa kuwapa matibabu hivyo kuipa mzigo Serikali.

Pia. Hamad aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchunguzwa afya zao utaratibu utakapokamilika, kwa kuwa yawezekana wapo baadhi wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali bila kujitambua.

Naye mwakilishi wa taasisi hiyo, Dk Soud Mgaya alisema wanatarajia kufanya uchunguzi kwa wananchi ili kuwasadia kutambua mapema afya zao.

Dk Mgaya alisema katika zoezi hilo watachunguza maradhi mbalimbali ikiwamo saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi, shinikizo la damu, kisukari na ugonjwa wa macho na meno.

Alisema licha ya uchunguzi huo kutakuwa na utaratibu wa uchangiaji wa damu salama.

Alisema katika zoezi hilo madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ndio watakaoendesha uchunguzi huo na kwamba, imekuwa bahati kwa wananchi wa Zanzibar hivyo awajitokeze kwa wingi.

“Mtu anapotambua mapema ugonjwa unaomsumbua humsaidia kuanza matibabu na magonjwa mengine yanatabika iwapo mhusika atapata huduma mapema,” alisema Dk Mgaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz