Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SADC yasema mipango manunuzi ya dawa ya pamoja imeiva

Wed, 14 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imesema  iliichagua nchi ya Tanzania kushughulikia ununuzi wa dawa wa pamoja (SPPS) baada ya kukidhi vigezo, malengo ikiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu kwa bei nafuu, bora na salama.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Agosti 12, 2019 na Mkurugenzi wa jamii na maendeleo ya watu kutoka SADC, Duduzile Simelane amesema wakati akieleza mchakato huo ulioamuliwa na baraza la mawaziri Novemba mwaka 2017 nchini Afrika Kusini.

Amesema manunuzi hayo ya pamoja yalitiliwa saini ya mkataba wa makubaliano mwaka 2018 kati ya Bohari ya Dawa (MSD) na Sekretarieti ya SADC  na mara moja walianza kuandaa rasimu ya mpango wa utekelezaji wa manunuzi.

“Tanzania ilichaguliwa na nchi wanachama kuratibu na kusimamia manunuzi ya pamoja na hatua hii ilifuatia malengo ambayo SADC ilijiwekea katika kuhakikisha inatibu kikamilifu magonjwa ambayo yana wasiwasi mkubwa kwa afya ya umma na tulilenga kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji endelevu wa upatikanaji wa dawa muhimu za bei nafuu, bora na salama,” amesema Simalane.

Simalane amesema tayari mipango kadhaa imekamilika katika mchakato huo ikiwemo miongozo ya rasimu ya SADC na taratibu zote za manunuzi zimeshakamilika.

Akizungumzia suala la udhibiti na kuoanisha sheria za manunuzi ya dawa na vifaa tiba, Simalane amesema ili kuboresha upatikanaji wa dawa kupitia mpango wa pamoja kikanda wa kisheria na mifumo, miongozo na michakato miongoni mwa wanachama SADC kupitia sekretarieti kwa kushirikiana na NEPAD na Benki ya Dunia kwa kufanya kazi na Mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini Zimbabwe (MCAZ).

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz