Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruksa watoto wenye miaka 5-11 kuchoma chanjo ya BioNTech-Pfizer

Student Getting Vaccinated Ruksa watoto wenye miaka 5-11 kuchoma chanjo ya BioNTech-Pfizer

Fri, 26 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Madawa la Ulaya na mdhibiti wa Dawa kutoka Umoja wa Ulaya wameidhinisha matumizi ya chanjo ya BioNTech-Pfizer, inayojulikana pia kama Comirnaty, kwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 11.

Hii inakua chanjo ya kwanza kuidhinishwa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.

Tayari Chanjo hiyo ilipata kibali cha kutumika kwa watoto wenye kuanzia miaka 12 tangu mwezi wa Tano mwaka 2021.

EMA imesema chanjo hiyo inapaswa kutolewa kwa watoto katika dozi mbili za mikrogramu 10 kwa wiki tatu tofauti kama sindano katika sehemu ya juu ya mkono. Ikumbukwa kuwa Dozi za watu wazima zina mikrogram 30.

Taasisi hizo zimesema majaribio ya kimatibabu ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 11 yameonesha kuwa chanjo yao ni nzuri na salama kwa 90.7% dhidi ya virusi vya Corona.

Idhini hiyo inakuja wakati Ulaya inapambana na ongezeko lingine kubwa la maambukizo ya COVID-19. Mamlaka nchini Austria, imetangaza kupata kiwango cha juu sana cha kesi za COVID, na haikungoja idhini ya EMA na tayari wameanza kutoa chanjo hiyo kwa watoto wa miaka 5 hadi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live