Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rufaa za Wagonjwa nje ya nchi zamalizwa

Dkt Mollel Awasimamisha Kazi Mganga Mkuu, Mganga Mfawidhi.jpeg Rufaa za Wagonjwa nje ya nchi zamalizwa

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rufaa za Wagonjwa nje ya nchi zamalizwa

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi ya Trilioni 6.7 katika sekta ya afya ili kuhakikisha anamaliza Rufaa za Wagonjwa wa nje ya nchi.

Dkt. Mollel amesema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika mbio za Saifee (SAIFEE MARATHON) zilizoandaliwa na Hospitali ya Saifee katika viwanja vya Green Park Masaki, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwezesha upasuaji wa Saratani ya Matiti kwa wanawake nchini.

Dkt. Mollel amesema kuwa ili kufikia azma hiyo Dkt. Samia ameboresha miundombinu katika sekta ya afya ikiwemo teknolojia katika sehemu ya kutolea Huduma, Upatikanaji wa dawa, pamoja na kusomesha wataalamu wa afya chini ya Programu ya Samia Scholarship.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamisi amesema kwa upande wa Zanzibari wameanza kushirikiana na Sekta binafsi na Hospitali ya Saifee inasimamia kuhakikisha Huduma za afya Zanzibar zinapatikana kwa ufasaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live