Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti: Mpango wa kutokomeza HIV, Malaria, TB

Hiv Erts Ripoti: Mpango wa kutokomeza HIV, Malaria, TB

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya kimataifa ya Global Fund imeonyesha wasiwasi katika mpango wa kutokomeza magonjwa ya Ukimwi, kifua kikuu na malaria kunakochangiwa na mabadiliko ya tabianchi.

Katika ripoti yao mpya iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 18, 2023, taasisi hiyo inasema mabadiliko ya tabianchi na migogoro duniani, vinakwamisha juhudi za kimataifa za kupambana na magonjwa hayo matatu.

Ripoti ya taasisi hiyo ambayo ni mfuko wa kimataifa wa kupambana na maradhi hayo, inaonesha kwamba japokuwa miradi ya kupambana na Ukimwi, malaria na kifua kikuu imerejea kote duniani baada ya kuathiriwa na janga la virusi vya Uviko, lakini hivi sasa inakabiliwa na vikwazo vinavyotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na migogoro.

DW imeripoti kuwa kiongozi wa taasisi hiyo, Peter Sands amesema majanga ya kimazingira mfano wa mafuriko, licha ya kwamba yanaongeza idadi ya wagonjwa, lakini pia yanasabisha kuwepo ugumu katka kuwafikia wagonjwa kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande mwingine, ripoti hiyo imesema ongezeko la joto pia limefanya ugonjwa kama malaria kusambaa hata kwenye maeneo ambayo hapo awali hayakuwa na matukio ya maradhi hayo.

Bosi huyo wa mfuko huo amesema, hali inayoendelea sasa inatishia malengo ya kutokomeza magonjwa hayo matatu ifikapo mwaka 2030.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live