Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Red Cross waja na mfumo mpya kuwasaidia waathirika wa maafa

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Red cross), kimebuni mfumo mpya wa uwasilishaji fedha kwa wahanga wa maafa mbalimbali utakaokwenda sambamba na utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa waliokumbwa na matatizo hayo.

Awali, Redcross ilikuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo magodoro, vyandarua kwa waathirika wa maafa ikiwemo mafuriko, lakini sasa hivi msaada huo utaenda na fedha zitakazotolewa kwa kaya husika.

Akizungumza leo Jumatano Juni 25,2019 na waandishi wa habari mkurugenzi wa kitengo cha maafa cha Red cross, Renatus Mkaruka amesema njia hiyo itakuwa bora zaidi na itawanufaisha waathirika wa maafa.

"Kwa kuanzia tutatoa Sh36 milioni kwa kaya  za 459 zilizopo kata za Kigogo na Tandale (Dar es Salaam) zilizokumbwa na mafuriko kwenye mvua za Aprili mwaka huu.Kila itapata Sh75,000 kwa awamu ya kwanza, lakini jumla wote kila kaya inatakiwa kupata 150000 sanjari na fedha ya kutolea," amesema Mkaruka.

Kabla ya kutoa fedha hizo, kaya hizo zilipewa misaada mbalimbali na Red cross ikiwemo magodoro na vyandarua wakati zilivyokumbwa na mafuriko Aprili mwaka huu.

Mkurugenzi Msaidizi wa maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu amesema utaratibu huo ni mzuri na utasaidia kaya kununua mahitaji wanayoyataka.

Pia Soma

"Nchi nyingine wanatumia mfumo kama huu, ambao gharama yake ni ndogo badala ya kununua vitu na kuanza kugawa kwa waathirika wa maafa mbalimbali," amesema Taratibu.

Chanzo: mwananchi.co.tz