Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi, Mloganzila sasa kujisimamia wenyewe

9d79cb69bc52468f746da649398f1d9e Rasmi, Mloganzila sasa kujisimamia wenyewe

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema kuanzia Julai mosi, mwaka huu, Hospitali ya Mloganzia, Dar es Salaam itajisimamia yenyewe.

Awali hospitali hiyo ilikuwa ikisimamiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lakini akizungumza leo wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema hospitali ya Mloganzila sasa inakuwa na uwezo wa kujisimamia yenyewe.

"Sasa tunataka Mloganzila isimame yenyewe kuanzia Julai mosi, 2022, tutaangalia ni maeneo yapi ambayo itahitaji kusimamiwa.

"Hospitali hii sasa ni miaka minne inasimamiwa na imetoa hadi huduma za kibingwa, hivyo ni vizuri kujisimamia.

Ummy ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuisimamia Mloganzila kwa wakati wote." Tunawashukuru Muhimbili, kama mtabadilisha jina tutajua tunafanyeje,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live